Ngono nzuri na tamu ni ipi..?

Ngono nzuri ni ile ambayo unajikuta umefanya ngono na mwanamme au mwanamke bila kuwa na wazo lolote kuhusu ngono, bila kuwa na hisia yoyote kuhusu ngono, wote wawili hamkuwaza kuhusu ngono, hamkupanga, hamkuwa na ahadi yoyote ya kufanya ngono, mnajikuta tu mmefanya.

Ngono ya aina hii ni nzuri sana, inaleta furaha, inaleta burudani ya pekee, nguvu chanya (mwanamme) na nguvu hasi (mwanamke) zinakutana bila uwepo wa akili. Jambo hili hutokea kwa nadra sana. Inawezekana jambo hili halijawahi kukutokea, na kama limeshawahi kukutokea utakubaliana na hayo niliyoyasema, utakuwa shahidi wa hayo niliyoyasema.

Lakini ngono zinazofanyika siku hizi ni zile za ahadi, ni zile za kupanga zifanyike kesho,wiki ijayo au mwezi ujao. Ngono hizi hufanyika bila hisia yoyote ya upendo, hufanyika kwa kuiwaza akilini kwanza, unaweza kufanya ngono na mwanamke bila kuwa hisia yoyote ya upendo, pia unaweza kufanya ngono na mwanamme bila kuwa na hisia yoyote ya upendo.

Huku ni kumtumia mwingine kama chombo cha starehe, huu ni ukahaba. Hali hii pia ipo sana kwenye ndoa. Unakuta mme na mke wanafanya ngono huku wakiwa hawana hisia yoyote ya upendo. Hii haina tofauti na kufanya mapenzi na kahaba, ingawa tofauti yake ni moja tu, nayo ni kwamba kahaba ni mbunifu zaidi, yupo hai zaidi kingono, hajakandamiza. Ngono ya aina hii siyo ngono, haiwezi kuwa nzuri, haiwezi kukupa furaha wala burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *